Friday, April 24, 2020

Mkuu wa WHO Afrika akosoa kasi ya Tanzania kuchukua tahadhari

mAGUFULI
Kuchelewa kwa Tanzania kuchukua hatua kali za kukabiliana na kusambaa kwa maambukizi ya corona kunatajwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama sababu ya kuongezeka kwa wagonjwa nchini humo.
Mkuu wa WHO wa bara la Afrika Bi Matshidiso Moeti anasema kuwa kumekuwa na hofu juu ya kukua kwa kasi ya maambukizi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
"Kwa hakika tumeona kuwa watu kuaacha kuchangamana, pamoja na kupiga marufuku kwa mikusanyiko ya watu wengi kumechukua muda mrefu kufanyika na tunaamini kuwa hayo yanaweza kuwa ni moja ya mabo yaliyopelekea ongezeko la kasi la wagonjwa wa corona," ameeleza Dkt Moeti katika mkutano na wanahabari.
Tanzania kwa mara ya kwanza iliripoti mgonjwa wa kwanza wa corona Machi 16 na kufikia sasa idadi ya maambukizi imefikia 284.
Baada tu ya kuripotiwa kwa ugonjwa huo, serikali ya Tanzania ilitangaza kufungwa kwa shule na vyuo vikuu pamoja na matukio ya kukusanya watu wengi kama ligi za michezo ikiwemo mpira na matamasha ya muziki.
Hata hivyo, serikali ya rais John Pombe Magufuli imekosolea vikali kwa kutochukua hatua kali kama kufunga (lockdown) vitovu vya maambukizi kama miji ya Dar es Salaam na Zanzibar.

Jumatano, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli liweka wazi kuwa serikali yake haitalifungia jiji la Dar es Salaam.

Licha ya Dar es Salaam kuwa kitovu cha maambukizi, Magufuli amesema jiji hilo la watu milioni sita ndio moyo wa mapato ya Tanzania.
"Wapo wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salaam, hili haliwezekani. Dar es salam ndio centre (sehemu) pekee ambapo collection (makusanyo) ya revenue (mapato) inapatikana kwa nchi yetu...Zaidi ya asilimia 80 ya mapato yanakusanywa Dar es Salaam," alisema Magufuli alipokutana na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo Jumatano.
Pia alisisitiza kuwa kutokana na wingi wa wakaazi wake, ilikuwa ni jambo la kutegemewa kitakwimu kwa jiji hilo kuwa na wagonjwa wengi zaidi.
Awali asubuhi ya siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Kassim Majaliwa akiongea kwenye ibada ya kuiombea nchini hiyo alisema anatambua kwamba kuna Watanzania ambao wanataka serikali ichukue hatua nyingi zaidi kudhibiti maambukizi ya virusi, lakini ameonya kuwa kila hatua ina faida na hasara zake.
"Ni vyema wajue kila hatua ina faida na hasara zake...Serikali inaendelea kutathmini kila hatua kwa faida na hasara zake kwa jamii. Ni vyema Watanzania mkaendelea kuiamini serikali, kuwaamini wataalamu wetu katika kuchukua hatua ambazo haziwezi kuleta athari zaidi kwa taifa."

Hatuazilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ni 

  • Shule zote na vyuo vya elimu vimefungwa mpaka itakapotangazwa ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona nchini humo.
  • Pamoja na kuzuia mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.
  • Magari ya usafiri wa umma hatayakiwi kujaza abiria, na wote lazima wawe wameketi vitini.
  • Ndege za abiria zimezuiwa kutua nchini humo.
  • Kuanzia Jumatatu ya Aprili 20 ni lazima kwa wakaazi wote wa Dar es Salaam kuvaa barakoa wanapokuwa maeneo ya umma.
  • Biashara zote za chakula jijini Dar es Salaam zinatakiwa kufunga bidhaa zao na kutoruhusu watu kula kwenye migahawa.

No comments:

Post a Comment