
Wizara ya afya nchini Uganda imetangaza wagonjwa wanne wapya wa virusi vya corona na kufanya idadi ya wanaothirika na ugonjwa huo kufikia 79.
Wagonjwa hao wanne ni madereva wa malori kutoka Tanzania waliowasili nchini humo kupitia mpaka wa Mutukula.
Wagonjwa hao ni miongoni mwa sampuli 1,578 zilizochukuliwa kutoka kwa madereva wa malori.
Kati ya sampuli za wakaazi 411 zilizochukulia ili kufanyiwa vipimo hakuna hata mtu mmoja aliyekutwa na ugonjwa huo.
Hatua hiyo inajiri siku chache tu baada ya Uganda kuwarudisha nyumbani kwa lazima raia mmoja wa Tanzania na mwengine wa Kenya ambao walikutwa na virusi hivyo.
Uamuzi huo umedaiwa kuathiri uhusiano kati ya mataifa hayo wanachama wa Afrika mashariki na hivyobasi kuhatarisha usafirishaji wa mizigo kati yao.
Kufurushwa huko ambako ni kinyume na mwongozo wa shirika la Afya duniani WHO kuhusu jinsi ya kukabiliana na majanga kama vile Covid-19 pia, umeliweka katika ratili soko huru la Afrika mashariki.
Uganda imedaiwa kuwarudisha nyumbani kwa lazima dereva hao wa malori ambao walikutwa na virusi vya corona , huku jopo lililoundwa nchini Sudan Kusini kukabiliana na Covid-19 likiamua kuwafurusha Wakenya wawili kwa kutumia ndege kulingana na gazeti la The East African .
Dereva mwanamume mwenye umri wa miaka 27 alikutwa na virusi hivyo kati ya madereva 372.
Sampuli yake ilichukuliwa katika kituo cha kibiashara kilichopo mpakani cha Malaba na anatarajiwa kurudishwa nyumbani ili kupatiwa matibabu.
Idadi ya malori yanayoingia Uganda kwa siku
Huku takriban malori 1000 ya mizigo yakidaiwa kuingia katika taifa hilo kwa siku, Madareva wa malori ya masafa marefu wamekuwa wasiwasi mkubwa nchini Uganda baada ya kuthibitishwa kuwa chanzo kikuu cha ugonja huo miongoni mwa raia wa kigeni.
Kati ya visa vipya vya Covid vilivyotangazwa nchini Uganda siku ya Ijumaa, wagonjwa sita walikuwa madereva wa malori kutoka Tanzania waliowasili kupitia mpaka wa Mutukula huku madereva wengine watano wakidaiwa kutoka Kenya waliongia kupitia mpaka wa Malaba na Busia.
Idara ya Afya nchini Uganda inayosaidiwa na vikosi vya usalama imedaiwa kumsaka dereva wa lori wa Tanzania ili kumrudisha nyumbani kwa matibabu.
Tukio jingine ni la dereva mwengine wa malori raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 34 kutoka Dar es Salaam ambaye aliwasili katika mpaka wa Mutukula tarehe 16 Aprili na ambaye hakuonyesha dalili zozote za Covid-19.
Kenya imekuwa ikiwatibu baadhi ya raia wa kigeni wanaokutwa na virusi hivyo kulingana na kaimu mkurugenzi wa huduma ya afya Dkt Patrick Amoth.
''Tumewatibu wagonjwa wengi wa mataifa ya kigeni kutoka Cameroon, Pakistan, Burundi na DRC . Kama taifa hatujaona sababu ya kuwatimua kutokana na hatari zinazohusishwa na usafiri wakati mtu anapougua virusi hivyo'', alisema Dkt. Amoth.
''Inashangaza mtu kufanya uamuzi kama huo kwasababu unaweza kuwaambukiza watu wengi zaidi unapomruhusu muathiriwa wa virusi vya corona kusafiri mbali wakati ambapo ingekuwa bora kumtibu katika taifa alilokutwa na virusi hivyo''. Aliongezea.
Museveni amesema baada ya kushughulikia ipasavyo mipaka ya anga, sasa hatua inayofuata ni kushughulikia pia mipaka ya ardhini na nchi jirani ili kuendelea kuzuia kasi ya maambukizi.
Maafisa waandamizi wa serikali ya Uganda wamekuwa wakinukuliwa kuwa wanataka madereva kutoka Kenya na Tanzania kuacha magari mpakani.
Baada ya kuyaacha hapo yatachukuliwa na madereva wa Uganda ambao watayapeleka mpaka mwisho wa safari. Museveni amethibitisha mpango huo akisema mawaziri wa afya wanaujadili
"Kubadili madereva, Madreva kutoka Kenya waendeshe mpaka mpakani kisha magari kupulizwa dawa na madereva wengine (wa Uganda) kuyachukua kutokea hapo. Hili pia mawaziri watalijadili," ameema Museveni.
Pia Uganda inataka madereva hao kupimwa kabla ya kutoka katika nchi zao.
Hatua nyengine ambayo Uganda inapanga kuitekeleza kwa sasa ni kuhakikisha wanawapima madereva wote kutoka nchi jirani na kuwaruhusu kuendelea na safari pale tu majibu yatakapotoka na kuonesha hawana maambukizi.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda Jenerali Jeje Odongo aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali ilikuwa inapanga kutumia vipimo vya haraka kuwapima madereva hao.
"Vipimo vya haraka vinatumia dakika 10 tu kutoa majibu, lakini changamoto yake ni kuwa kipimo kimoja ni dola 65 na kwa wastani siku moja magari 1,000 huingia Uganda.
Amri ya kutoka nje Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma.
Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni Bw. Museveni alipiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.
Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani
Wauzaji bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao kuuzia bidhaa zao .
Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.
No comments:
Post a Comment