Dar es Salaam. Nyota kikapu zamani wa timu ya L.A Lakers, Marekani Kobe Bryant amefariki dunia pamoja na wenzake wanne kwenye ajali ya helikopta iliyotokea California usiku wa kuamkia leo tarehe 26 Januari 2020.
Taarifa kutoka Marekani zimeeleza kuwa Kobe Bryant alikuwa akisafiri kwa helikopta binafsi kabla haijalipuka na kuteketea kwa moto huko Calabasas.
Kwa mujibu wa Mamlaka jijini Los Angeles wameeleza kuwa jumla ya watu watano walikuwa kwenye helikopta hiyo na hakuna aliyenusurika katika ajali hiyo.
Kobe Bryant amefariki akiwa na umri wa miaka 41 akiwa na ameichezea timu ya mpira wa kikapu ya Los Angeles Lakers nchini Marekani kwa takribani miaka 20, hadi alipostaafu mwezi Aprili mwaka 2016
Miongoni mwa mafanikio ambaye Kobe Bryant alifanikiwa kuyapata ni pamoja na kuwa Mcheza kikapo mwenye thamani kubwa mwaka 2008, na mara mbili pia alikuwa ndiye mchezaji mwenye thamani hiyo kwenye fainali ya ligi ya NBA

No comments:
Post a Comment